Duration 12:42

NAFASI YA ULIMWENGU WA NDOTO KWENYE MAISHA YA MTU - SEHEMU YA TATU

3 864 watched
0
97
Published 14 Nov 2021

Mwanzo 37:8 [8]Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Katika somo hili tutaangalia zaidi ndoto katika upande wa maono uliyonayo juu ya maisha yako.Kuna maono ambayo Mungu ameyaweka ndani yako,na siku zote maono haya huwezi kuyatimiza peke yako,kuna watu ambao Mungu anakuwa amewaandaa kwa ajili ya kuhakikisha unafika pale ambapo amekuitia kufika. Kilichomfanya Yusufu achukiwe zaidi na ndugu zake sio tu kwa sababu ya ndoto au tafsiri ya ndoto pekee bali pia kutokana na namna alivyoiwasilisha hiyo ndoto,ndio maana Neno la Mungu linasema kuwa "..Wakazidi kumchukia kwa sababu ya ndoto yake,na kwa maneno yake". Hapa utaona kuwa kuna namna ambavyo Yusufu aliwasimulia ndugu zake juu ya ndoto na ni namna ambayo sio nzuri.Unapomuelezea mtu juu ya maono uliyonayo unamuelezea vipi?maana maelezo unayotoa ndio yamebeba picha ya ukubwa wa hayo maono,kwa uwasilishaji wako watu wanaweza wakakushika mkono au wakakukataa. Mungu akupe neema ya kuwakilisha maono sahihi,kwa namna sahihi,mbele ya watu sahihi. #PastorSubellaKyando#Ulimwengu#WaNdoto

Category

Show more

Comments - 8