Duration 8:18

Mtoto kucheza chini ya Kitovu ktk Tumbo la Mjamzito ina maanisha Nini | Je ni Dalili ya hatari.

87 037 watched
0
785
Published 16 Dec 2021

MTOTO KUCHEZA CHINI YA KITOVU HUMAANISHA NINI? JE NI KAWAIDA? Ukweli ni kwamba Mjamzito anayebeba Mimba kwa Mara ya kwanza huanza kuhisi Mtoto kucheza Wiki ya 18 hadi Wiki 20 kwenda juu, Mjamzito ambaye anabeba Mimba kwa Mara ya Pili,Ya Tatu au zaidi huweza kusikia Mtoto anacheza kuanzia wiki ya 16 hadi 18 kwenda juu. SABABU ZINAZOPELEKEA MTOTO KUCHEZA CHINI YA KITOVU KTK TUMBO LA MJAMZITO. Kuna sababu kuu Mbili ambazo hupelekea Mjamzito kuhisi Mtoto anacheza sehemu ya chini ya Tumbo yaani chini ya Kitovu haijalishi upande wa Kulia au Kushoto sehemu ya chini ya Kitovu. 1. Umri wa Mimba/Ujauzito. Kwa kawaida Wanawake wengi huanza kusikia Mtoto akicheza Mimba ikifikisha Wiki 16 hadi Wiki 20 ndio kipindi ambacho Wajawazito wengine husikia Mtoto akicheza Chini ya Kitovu ktk Tumbo lao, Mjamzito ambaye ana Mimba chini ya Wiki 22 au Miezi Mitano na Wiki 2, Mara nyingi husikia Mtoto akicheza Chini ya Kitovu hii ni kwa sababu Mimba inapofikisha Wiki 20 Mji wa Uzazi huwa umefika kwenye Kitovu na sehemu ya chini ya Tumbo hususani sehemu ya chini ya Kitovu, Ndio maana kwa asilimia nyingi Mtoto hucheza chini ya Kitovu. 2. Mkao wa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito. Hii huwa zaidi kwa Wajawazito wenye Mimba kuanzia Wiki 22 kwenda juu, Kumbuka sehemu ambazo Mtoto huchezesha au huwa na Mtikisiko zaidi akiwemo ni Miguu na Mikono ya Mtoto. Hivyo wakati mwingine Mtoto anapocheza kwenye Tumbo la Mjamzito inawezekana kabisa kujua Mtoto amekaa Mkao upi katika Tumbo la Mjamzito. A. Mtoto aliyegeuza Kichwa chini (Cephalic Presentation) Endapo Mtoto amegeuza Kichwa Chini inategemeana zaidi na alivyogeuza Miguu na Mikono yake lakini huweza kupelekea Mtikisiko wa Tumbo Sehemu ya juu ya Kitovu, sehemu ya katika ya Kitovu au Pembeni mwa Tumbo yani Kushoto au Kulia. B. Mtoto aliyekaa kwa Ulalo. (Transverse Lie) Endapo Mtoto amekaa Ulalo maana yake Mikono na Miguu inawezekana ikawa upande wa Kushoto au Kulia hivyo sehemu zitakazokuwa na Mtikisiko zaidi ni upande wa Kushoto, katikati au Kulia mwa Tumbo la Mjamzito. C. Mtoto aliyetanguliza Matako/Makalio. ( Breech Presentation) Endepo Mtoto ametanguliza Matako inawezekana akawa anacheza zaidi chini ya Kitovu lakini hutegemea zaidi Aina ya Breech endapo ametanguliza Makalio na amekunjua maungio ya kwenye goti (Frank Breech) huweza kuwa anacheza zaidi upande wa juu wa Tumbo, Kushoto sehemu ya juu ya Kitovu au Kulia sehemu ya juu ya Kitovu katika Tumboni mwa Mjamzito wakati mwingine sehemu ya katika mwa Tumbo la Mjamzito (Kitovuni) KUMBUKA: Ili uweze kujua mkao wa Mtoto unatakiwa kwenda hospital ukachunguzwe na wahudumu wa Afya ambapo watakagua Tumbo lako na kujua kuwa Mtoto amekaaje Tumboni au Unaweza kufanya Ultrasound na itakusaidia kujua mwanao amekaaje Tumboni. Endapo Mtoto ametanguliza Makalio na Mimba haijafikisha Wiki 36 basi haina shida na hutakiwi kuwa na hofu, kwa sababu Mtoto anakuwa Breech au Ametanguliza Makalio endapo Mimba imefikisha wiki 36 kwenda Juu na hii huweza kupelekea changamoto wakati wa Kujifungua. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp #MtotoKuchezaTumboni #DrMwanyika #MamaAfya

Category

Show more

Comments - 396