Duration 3:40

HUDUMA ZA RUFANI ZAANZA KUTOLEWA MAHAKAMA KUU SHINYANGA

234 watched
0
2
Published 9 Aug 2020

#MhakamaKuu #Rufani #Shinyanga Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma amesema mwaka huu mahakama kuu ya Tanzania inatimiza miaka mia moja na ilianzia Jijini Dar es Salaam na kwa sasa imefungua matawi yake katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Mkoa wa Shinyanga. Profesa Juma amesema hayo mapema leo Mkoani Shinyanga katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga na kuongeza kuwa Mkoa huo umekuwa na bahati ya kuwa na jengo la kisasa la mahakama kwani bado kuna mikoa mingi sana ambayo haina Jengo la Makao Makuu. Aidha Kiongozi huyo Mkuu wa Mahakama ya Tanzania amesema uwepo wa mahakama hiyo ya kisasa mkoani Shinyanga inamaanisha kuleta huduma karibu kwa wananchi kwakuwa uwepo wa wananchi ndio unafanya wataalam wa kada ya sheria kuendelea kuwepo. Jaji Mkuu amesema kuwa pamoja na ujenzi wa jingo la Mahakama Kuu lakini ndani ya Jengo hilo kutakuwa na huduma za rufani hivyo kuwaondelea wananchi wa Shinyanga kufuata huduma hizo jijini Dar es Salaam au mahali pengine nje ya mkoa wa Shinyanga. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kuwezesha ujenzi wa jengo hilo Mkoani Shinyanga na kuongeza kuwa jengo hilo la kisasa linawezesha Majaji kufanya kazi yao kwa weledi na bila usumbufu wote na hivyo kuongeza ufanisi katika utendaji haki hapa Nchini. Bi. Telack pia amesema jingo hilo la kisasa ni jengo la kutoa haki kwa wananchi wa Shinyanga ambao awali walikuwa wanafuata huduma ya kesi za rufani Mkoani Tabora na sasa huduma hiyo inapatikana Mkoani Shinyanga na haki inatendeka jambo ambalo limetupa heshima kama mkoa wa Shinyanga. Wakati huo huo Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mohamedi Chande Othman amesema kuwa Mahakama inapojenga majengo inasogeza huduma karibu kwa wananchi na kuongeza kuwa jambo hilo na la kihistoria kwani wakoloni hawakuwa na haja ya kujenga miundombinu ya mahakama na sasa suala hilo limekuwa likifanyika kwa awamu toka Nchi kupata uhuru. Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande ameongeza kuwa uwepo wa matumizi ya teknolojia ya kisasa utaongeza ufanisi wa Mahakama Nchini inatoa fursa ya utendaji kazi bora wa sekta ya Mahakama hapa Nchini.

Category

Show more

Comments - 0