Katika kuhakikisha wafanya kazi wanatekeleza majukumu yao katika mazingira yanayolinda usalama na afya zao, OSHA ilifika katika kampuni ya Amboni Plantations iliyoko Pangani mkoani Tanga kwa lengo la kufanya ukaguzi, kutoa elimu pamoja na kuendesha zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.