Duration 3:8

KESI YA IDRIS SULTAN: MASHAHIDI 15 KUSIMAMA KIZIMBANI, ASOMEWA MAELEZO YA AWALI

2 912 watched
0
20
Published 9 Jul 2020

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Agosti 5, mwaka huu kuanza kusikiliza jumla ya mashahidi 15 katika kesi inayomkabili msanii Idris Sultan ya kushindwa kusajili laini ya simu iliyokuwa inamilikiwa na mtu mwingine. Mbali ya Idris, mshitakiwa mwingine ni Innocent Maiga. Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ambapo alianza kwa kumsomea upya mashitaka yanayomkabili. Amedai kati ya Desemba 1, 2019 na Mei 19, 2020 katika eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Idriss alitenda kosa la kushindwa kufanya usajili wa laini ya simu inayotumiwa na mtu mwingine. Inadaiwa katika kosa hilo mshitakiwa alitumia kadi ya simu iliyomilikiwa na Innocent Maiga bila kuripoti kwa mtoa leseni. Katika shitaka jingine linamkabili mshitakiwa Maiga ambapo anadaiwa kutenda kosa la kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya kadi ya simu kutoka kwake kwenda kwa Idriss kosa analodaiwa kulitenda kati ya Desemba 1, 2019 na Mei 19, mwaka huu eneo la Mbezi Beach Kinondoni jijini Dar es Salaam. Pia inadaiwa Mei 5, mwaka huu Mkuu wa Upelelezi Kinondoni alipewa taarifa kwamba Idriss anatumia kadi ya simu ya Vodacom ambayo haijasajiliwa kwa jina lake na kwamba alitakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo alifanya hivyo. Ilidaiwa Polisi walienda kufanya upekuzi nyumbani kwa Idriss na kubaini uwepo wa laini hiyo ya simu na kwamba alikuwa akiitumia kwa mawasiliano yake ya kila siku licha ya kusajiliwa kwa jina la Maiga. Inadaiwa Idriss alikiri kutumia kadi hiyo ya simu ambayo ilikuwa ikimilikiwa kabla na Maiga na kwamba alikiri kuitumia tangu Desemba mwaka jana. Mshitakiwa Maiga anadaiwa kukiri kumiliki kadi hiyo na alimpatia Idriss aweze kuitumia na kwamba alikiri kutoripoti kwenye mamlaka kuhusu mabadiliko ya kadi hiyo. Hata hivyo, washitakiwa hao ambao wanawakilishwa na Wakili Jebra Kambole na Maria Mushi, walikiri maelezo yao binafsi pamoja na mashitaka yanayowakabili mahakamani hapo na kukana maelezo ya mashitaka. Upande wa mashitaka umedai wataleta mashahidi 15 na kama watahitaji kuongeza au kupunguza mashahidi wataieleza mahakama na kwamba wataeleza idadi ya vielelezo watakavyokuwa navyo kesi itakapoendelea.

Category

Show more

Comments - 4