Duration 13:3

WAFUGAJI WA KANDA YA ZIWA WAANZA KUNUFAIKA NA NDEGE ZA DREAMLINER

470 watched
0
4
Published 7 Jan 2019

Wakulima wa mkoa wa Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla kunufaika na uwepo wa ndege za shirika la ndege nchini (ATCL) baada ya kampuni ya Chobo investiment ya mkoani humo, kuanza kusafirisha Nyama kupeleka nchini Dubai kutoka Mwanza kupitia uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Akishughudia usafirishaji huo mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amesema uwepo wa ndege hizo zilizonunuliwa na serikali ya awamu ya tano itamnufaisha kila mwananchi kwa nafasi yake hivyo amewataka wananchi kutumia fursa ya uwepo wa ndege hizo kujinufaisha kiuchumi. Naye mnunuzi wa Nyama hizo kutoka nchini dubai ..AL FALAZ ameshukuru serikali ya Tanzania kwa kununua ndege hizo kwani sasa atachukua siku moja pekee kufikisha Nyama hizo kwenda nchini Dubai tofauti na awali ambapo alilazimika kutumia hadi siku tatu kusafirisha mzigo huo toka kiwandani, huku mmiliki wa kiwanda cha Chobo investiment JOHN CHOBO akihaidi kushirikiana na uongozi wa mikoa kutoa elimu kwa wafugaji ili waweze kunufaika na fursa hiyo.

Category

Show more

Comments - 4